BITCOIN : Adui Wa Mabenki Duniani | Mwanzilishi hajulikani | Whitepaper

 


Mwaka 2008 Mtu asiyejulikana anakuja na wazo kubwa la kuibadili dunia kwenda katika njia Tofauti kabisa 

Binadamu huyu wa Tofauti anajulikana kama Satoshi Nakamoto ,Jina ambalo mpka leo hajulikani mmiliki wake


k31 October 2008 kupitia website ya bitcoin.org inaachiwa ujumbe mzito ambao unaelezea kiundani kuhusu BITCOIN


Mwaka 2009 Anafanikiwa kutumia teknolojia ya juu sana inayojulikana kama blockchain na kutengeneza pesa ya kidigitali baada ya kufanya mining ya genesis block 


pesa ya kidigitali inapewa jina la BIT coin (Bitcoin) pesa ambayo huwezi kuishika lakini ina nguvu kama zilivyopesa za Makaratasi 


Ujumbe huu wenye kichwa cha habari A PEER TO PEER ELECTRONIC CASH SYSTEM unazidi kuingia masikioni mwa watu, watu wanaanza kubadilishana piza na bitcoin 


Baadae Exchanges za kununua bitcoin zinaanza kuongezeka, Bitcoin inaanza kwa na thamani ya kujulikana kwa watu 


Hatimae Pesa ya kidigitali au cryptocurrency inaanza kutumiwa na watu wengi zaidi na kupata nguvu na badae cryptos zingine zinaanza kutengenezwa 


Lakini bado bitcoin anazidi kuwa baba yao kwa ukubwa wa market cap na hata thamani yake 


KWANINI BITCOIN ANAKUWA ADUI WA MABENKI 

Hii ni kwasababu ya peer to peer electronic cash yaani mfumo ambao unafanya watu watumiane pesa za kidigitali bila intermediate (Mtu kati) 


Kama unaweza kutuma pesa bila Mtu kati basi mabenki yatafanya nini ?


Mfumo huu wa fedha lazima utikise mabenki ambayo yanafanya kazi kama mtu kati, yaan ukituma pesa kwa mtu kupitia benki lazima yaupitie muamala kama ilivyo kwa Mpesa n.k


Nisiongee sana lakini hebu soma hiki ambacho Satoshi Nakamoto aliandika katika BITCOIN WHITE PAPER hiyo 
Reactions

Post a Comment

0 Comments