META VERSE : Maana yake| Historia yake | Je hii ndio Dunia Ijayo?

 


METAVERSE 
Hivi umewahi kufikiria sikumoja kwamba unaweza kwenda sehemu fulani bila kupanda gari, rocket au usafiri wowote na ukafika na kuinteract kiuchumi eneo hilo ? 


Unapo zungumzia dunia au maeneo ya kufikirika basi moja kwa moja unazunvumzia metaverse,Yaani mazingira mbali kabisa na haya tunayoyaona 

Neno Metaverse linaweza kuvunjwa katika sehemu mbili yaani META +VERSE. Meta ikiwa na maana ya Beyond na VERSE ikiwa ni UNIVERSE  ambayo ni jumla ya vitu vyote vinavyotuzunguka zikiwemo sayari nyota n.k 

Hivyo basi Metaverse ni dunia nyingine kabisa ya kufikirika ambayo miaka ya nyuma ilizungumzwa sana kupitia vitabu vya simulizi ndefu yaani NOVELS 

Mwandishi Neal Stephenson kupitia kitabu chake cha Snow crash aliweza kuzungumzia Metaverse hii ikiwa mwaka 1992 ,kitu ambacho kilipelekea uwepo wa games kama second life ambazo ziliruhusj kushiriki katika dunia za kufikirika kamma avatars 

UNAWEZAJE KUINGIA KATIKA DUNIA YA KUFIKIRIKA?
Kwa kutumia kifaa maalumu kinachojulikana kama VR headset ambacho kinavaliwa na kufunika macho kinamuwezesha mtu kuona mazingira mengine tofauti kama amabvyo yametengenezwa katika software mfano games software 

Kampuni mbalimbali zinajihusisha na kutengeneza hizi VIRTUAL REALITY (VR) headsets ikiwepo kampuni ambayo ilinunuliwa na mark Zuckerberg inayoitwa Oculus mwaka 2014 hii ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuwekeza zaidi katika Metaverse 

Hii imepekea pia siku chache hapa Nyuma kuweza kubadili jina la kampuni yake ya facebook na kuwa Meta (Metaverse platforms inc)  wakati huohuo tech giant mwingine MICROSOFT akionyesha kuwekeza pia katika Metaverse 

Ukiachana na metaverse kujulikana zaidi upande wa games, ujio wa cryptocurrencies na ukuaji wa blockchain technology umefanya Metaverse kuwa tamu zaidi na hii ndo imevuta zaidi kampuni nyingi kubwa kuanza kuwekeza kupitia vifaa lakini Metaverse tokens 

TOFAUTI YA METAVERSE NA CRYPTO METAVERSE 
Metaverse hii iliyofanya mpaka Facebook kubadili jina sio Metaverse: ya playstation wala novels, hii inajulikana kama crypto metaverse, Na hizi ndo Tofauti zake 

Decentalization ; Uwepo wa blockchain umefanya dunia sasa kuhama kutoka centralization na kuwa decentralization ambapo kampuni ambaye inahusika naomba software husika haitakuwa na uwezo wa  KUCONTROL maisha katika Metaverse husika (No intermediate ) 

Kuwa dentralized ina maana kuwa maamuzi hayapo chini ya mtu mmoja yaani minority bali katika wengi Majority kitu ambacho kimeweza kukua zaidi kupitia crypto games kama axie infinity 

Uwepo wa governance tokens : Hizi ni tokens ambazo ndizo zina influence zaidi katika maamuzi haswa katika kuamua ni nini kifanyike mbeleni katika Metaverse na hivyo watu kupiga kura mfano katika Metaverse token ya Decentraland 

Ambapo kupitia decentraland yoyote anaweza kununua ardhi na digital assets zingine na umiliki wake katika Mfumo wa NFTs na kuweza kuswap kuwa cryptos kitu kinachofanya kuwe na muunganiko wa Dunia ya kufikirika na dunia hii tunayoishi (Nitazungumzia NFTs siku nyingi lkn kifupi chake ni kuwa assets yoyote ikiwa stored kama NFT haiwez kumilikiwa na mtu mwingine 100%)

Hivyo basi kupitia crypto Metaverse watu wanaweza kutengeneza kipato katika virtual worlds na kukifanya kipato hicho kuwa na thamani pia katika dunia ya leo 

Ujio wa cryptogames na NFTs umepelekea ukuaji wa haraka sana katika soko la crypto Metaverse Metaverse ambapo mpaka sasa unaweza kuwekeza na kushiriki katika ulimwengu wa kufikirika kupitia tokens kama Decentraland, Metahero, sandbox za zingine 

Ni fursa kwa watu wengi kuwekeza katika crypto Metaverse mapema kwa kununua tokens na hivyo kushiriki katikat virtual world kiuchumi na kidemokrasia, Dunia inaelekea huko kwa kasi sana 

Imeandaliwa na kuandikwa na mimi @fradofx 

Reactions

Post a Comment

0 Comments