BIASHARA YA FOREX | DIAMOND VS ALIKIBA

KAMA FOREX INGEKUWA MZIKI JE NI NANI INGEMFAA ZAIDI ?

Kwanza Ningependa kutoa rai kuwa mimi sio shabiki wa Msanii Diamond wala Alikiba, na makala hii haijaandikwa kwa ushabiki


Tupo katika dunia ambayo kipaji hakitoshi kukufanya kuwa bora zaidi Kipaji bila juhudi binafsi hakiweza kumtengeneza best version of You 

Kama utakuwa unafatilia Muziki wa Bongo fleva basi utakuwa umeanza kunielewa


Ukweli ni kuwa Diamond anaonekana msanii ambaye anapambana sana na huku watu wengi wakisema Diamond hana kipaji kikubwa ukilinganisha na Alikiba 


Alikiba kamzidi Diamond kwenye Sauti kitu ambacho ni inborn na hiki ndio kipaji na silaha moja kubwa sana katika mziki, But Guess What ♡♡ ! Diamond ni Mkubwa zaidi internationally kuliko Alikiba 

Vigezo ambavyo naamini tutakubaliana kwenye ukubwa wa hawa wasanii ni upande wa Tuzo walizowahi kuwania na kuchukua,Followers katika mitandao ya kijamii,shows nje na ndani ya nchi, Gharama ya kuwapata,Utajiri wao katika mziki n k)Inshort Diamond ni mpambanaji, ana juhudi zaidi katika mziki na hata nje ya mziki kuliko Alikiba ambaye ame relax akiamini zaidi katika kipaji chake 


Katika biashara ya Forex uhitaji Kipaji, unahitaji juhudi, haijalishi una degree ya Finance au uchumi lakini ni lazima usukume, Kama kweli unataka kuwa profitable trader basi unatakiwa kutumia muda wako katika charts 


Haijalishi una masters ya uchumi ukirudi katika forex unatakiwa kuweka pembeni hiyo ego na kuanza kujituma, kuridhika kwa njia yoyote katika forex itakutoa njia kuu 


Unahitaji moyo wa Simba ili kutoboa katika comfort zone yako vilevile katika forex ni lazima uwe mpambanaji asiye kata tamaa, mwenye ndoto kubwa, mwenye kuamini kwamba anaweza na asiyerudishwa nyuma kwa losses 


Akili yako inatakiwa kutawala hisia zako ili kufikia pale unapotaka kufika katika biashara ya Forex


Mwisho kabisa : Sijaandika post hii kwa ushabiki,Mimi sio shabiki wa Alikiba wala Diamond lakini ni Shabiki ya Mziki mzuri 


Reactions

Post a Comment

0 Comments