Dogecoin itatengeneza mamilionea | FradoFxUkiachana na kile ambacho Dogefather Elon Musk alikisema kuhusu dogecoin, wiki hii imekuwa ya Mapinduzi makubwa sana upande wa Dogecoin 


Kupitia mtandao wa twitter developer maarufu anayejulikana kama inevitable360 aliweza kuweka wazi kuwa ameweza kufanya NFT minting kupitia Dogecoin blockchain 


inevitable360 alishare screenshot ya NFT (Non Fungible Tokens ) hizo


NINI MAANA YA NFT?

NFT inasimama kama Non Fungible Tokens ,Ili kuelewa maana ya NFT nitatumia mfano,Chukulia wewe una miliki nyumba na unataka kuiuza,Hivi ni kitu gani ambacho kinaonyesha umiliki wa hiyo Nyumba, hapo bila shaka ni hati ya nyumba 


Lakini katika ulimwengu wa digital hatuhitaji hati ya nyumba au makaratasi mengi kuonyesha kuwa Nyumba ni yako, Happ ndipo linakuja swala la NFTs (Non Fungible Tokens )


NFTs ni non fungible token ikiwa na maana ni non interchangeable token, kwanza kama utakuwa na physical asset kama Nyumba na ardhi katika metaverse unaweza kui mint kama NFT na ikawa stored katika blockchain ili mtu mwingine yoyote asije kujimilikisha(Hapo tunachukulia picha au video kama NFT)


Wasanii kama The weekend walitangaza pia kuanza kuuza nyimbo zao katika mfumo wa NFTs ili  kuepusha watu kuuza kazi zao bila wao kulipwa 


NFTs zina kitu kinaitwa Royalty ,Royalty ni asilimia ambayo mmiliki analipwa pale unapouza NFT yake ,mfano Baada ya Nike kumint viatu vya kama NFT walikuwa wanapokea 10% ya Mauzo kwa kila sales 


NFT inaweza kuwa katika mfumo wa picha, video n.k lakini Tofauti kubwa ikiwa ni lazima iwe stored katika blockchain kitu kinachoifanya itumike kama proof of ownership (hati ya umiliki )


SABABU ZINAZOFANYA NFT KUWA KITU KIKUBWA ZAIDI DUNIANI 


1- Ukuaji wa Metaverse 

Ujio mkubwa wa vurtual worlds (Dunia za kufikirika ) kama Metaverse, unafanya NFT kuendelea kuwa kitu kikubwa zaidi, Why? Kwasababu hakuna asset yoyote inawezwa kuuzwa bila ya kuuzwa kama NFTs,Uuzwaji mkubwa wa ardhi (virtual land ) katika decentraland na sandbox wote hufanyika katika mfumo wa NFT 2 –  Kuuza na kununua NFTs 

Hii imekuwa biashara kubwa sana ambapo NFTs collections kamata Bored Ape na cryptopunks zimetengeneza mamilionea wengi sana duniani, Celebrities kama Snoop Dog, Legan Paul na Gary vee tayari wameshatengeneza Mamilioni ya dola kupitia NFTs (Nitaekezea kwa undani zaidi siku moja hapahapa)


3 – Kupunguza wizi 

Ukiacha na NFT kutumika katika Metaverse hasa kuonyesha umiliki wa plots za viwanja, wasanii wengi wamekuwa hawapati faida wanayostahili katika kuuza albums na nyimbo zao 


Hebu chukulia umetoa album ina nyimbo 15 na uka burn copies Million 1 lakini baada ya Masaa 2 watu tayari wana nyimbo zako na hujarudisha hata pesa ya productions (No royalty ) kitu ambacho ni Tofauti na NFTs
MAHUSIANO YA THAMANI YA DOGECOIN NA NFT 

Kwanza kabisa soko la NFT linakuwa kwa kasi sana na kama NFT itaweza kuwa minted katika DOGECOIN blockchain basi watu wengi watakimbilia huku kutokana na makato madogo na hivyo watahitaji kununua DOGECOINS ili wafanye minting na hivyo thamani yake kupanda 


Japo DOGECOIN founder hajazungumza chochote kuhusu NFT minting katika dogecoin  blockchain officially Mr inevitable360 tayari atakuwa umefungua mlango wa watu wengi kuanza kufatilia hili


MAHUSIANO YA DOGECOIN NA TESLA 

Siku chache Nyuma Elon Musk aliweza wazi kuwa mwakani watu wataweza kununua gari zao kwa dogecoins kitu ambacho kitafanya watu wengi waweze kununua dogecoins ili baadae zitumike katika manunuzi hayo ili kupunguza makato pia 


NB : Ni vyema kufahamu utafiti wako pia kabla ya kununua cryptocurrency yoyote 

Ahsante sana kwa kusoma makala hii mpaka mwisho 


Written and edited by FradoFx 
Reactions

Post a Comment

0 Comments