Elon Musk | Dogecoin ni bora kuliko Bitcoin

 


Tajiri namba moja Duniani na influencer mkubwa zaidi katika soko la fedha za kidigitali (Cryptocurrency) Mr. Elon  Reeve Musk anazidi kuionyesha dunia kuwa yupo upande wa Dogecoin 


Katika mjadala na Times Magazine akiwa kama Man of the year, Elon Musk aliulizwa kuhusu maoni yake kuhusu bitcoin na Dogecoin 


Bila kupepesa macho Tesla and space X CEO alisema kuwa anaamini dogecoin ni bora zaidi kuliko bitcoins hasa katika kufanya miamala (Transactions )


Elon Musk aliongezea na kusema kuwa, kupitia dogecoin unaweza kufanya manunuzi kwa haraka zaidi kuliko bitcoin, katika upande wa transactions per speed Dogecoin ni chaguo sahihi


Elon Musk hakuishia hapo aliongezea pia kuwa miamala inayofanyika kupitia dogecoin ina makato madogo ukilinganisha na upande wa bitcoin 


Elon Musk pia aliongezea pia kuwa katika matoleo ya gari mpya za kampuni yake ya Tesla wateja wake wataweza kununua gari hizo kwa kutumia Dogecoins 


Makato ya kila muamala kupitia DOGECOIN yana uwiano wa dola za kimarekani 0.65 sawa na 1,495 za Kitanzania (source :coindesk)


Wakati makato ya kila muamala kupitia bitcoin yakikadiliwa kuwa 34,500 za kitanzania  (source : coindesk)


Ikimbukwe Elon Musk aliwahi kuruhusu wateja wake kufanya manunuzi kwa kutumia bitcoin hapo nyuma kabla ya kuipiga chini BTC na kuhamia dogecoin 


Moja ya sababu kuwa ni kuwa bitcoin inatumia  umeme mkubwa zaidi katika mining na hivyo gharama kubwa lakini pia uchafuzi wa Mazingira 


Kauli yake hiyo imeendelea kuifanya bitcoin kuendelea kuwa katika thamani ya Milioni 109 kwa kila coin mpaka sasa napoandika makala hii,hili likiwa anguko la asilimia 35


NB : Uli kuendelea kupata makala haya SUBSCRIBE wa kutumia email yako ili upate masomo haya katika inbox yako automatically kila Tunapoweka masomo mapya 


Mwandishi : Frank B Phillibert (FradoFx )


Reactions

Post a Comment

0 Comments