Elon Musk - Nilienda Marekani bila pesa yoyote


 Elon Reeve Musk ambaye ndiye tajiri mkubwa zaidi duniani Wiki hii ameshangaza watu wengi sana baada ya kuweka wazi ni namna gani alienda Marekani kama Mwanafunzi  


Akijibu tweet iliyoandikwa na ukurasa wa whole mars catalog kupitia twitter Elon anasema kuwa alienda Marekani kama mwanafunzi akiwa hana pesa na kumaliza akiwa na deni lisilopungua dola laki 1 za kimarekani japo alikuwa chini ya scholarship na akifanya kazi mbili nje ya masomo 


Whole Mars catalog walu tweet kuwa Elon musk akiwa na umri wa miaka 17 aliingia marekani ,Elon ameongeza pato la taifa kupitia kodi, ameongeza exports (usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi)Ameongeza usalama wa taifa, katengeza ajira na hata mamilionea 


Hii inaonyesh wazi kuwa hupaswi kukata tamaa,haijalishi upo katika hatua gani lakini unaweza kuanza na sifuri na ukawa mtu mkubwa sana bila kujali umezaliwa wapi au katika mazingira yapi


NB : Elon Musk ni mzaliwa wa Afrika Kusini ambaye ana Uraia pia Wa Marekani na Canada 

Reactions

Post a Comment

0 Comments