Fahamu kila kitu kuhusu NFT/maana ya NFT/Faida na hasara - (NFT Full guide)

 


NFT – NON FUNGIBLE TOKEN

Utangulizi

Dunia ipo kasi sana kutoka kwenye ulimwengu  centralized na kwenda Decentralised,hii ypte inatokana na ukuaji mkubwa wa teknolojia ya blockchain

 

Watu wengi wameendelea kuipenda teknolojia hii kutokana na uwezo mkubwa wa kuondoa intermediates(watu kati) katika miamala lakini pia usalama mkubwa

 

Blockchain ilianza kupata umaarufu kwa watu wa kawaida kuanzia mwaka 2009 baada ya kutumika katika utengenezaji wa mother cryptocurrency – BITCOIN

 

Ukiachana na teknioijia hii kutumika katika kutengeneza cryptocurrencies (pesa za kidigitali) kwasasa blockchaininazidi kupanuka Zaidi na kupitia teknolojia hii watu wanaweza kufanya minting/kutengeneza NFTs

 

NINI MAANA YA NFT?

NFT ni ufupisho wa neno Non Fungible token

Neno “Fungible” lina maana ya linaweza kubadilishwa –interchangle ,mfano nakupa nyumba na unanipa pesa na nyumba inakuwa mali yangu kwa asilimia 100 hivyo basi Non Fungible ina maana “haiwezi kubadilishwa na kitu kingine kwa asilimia 100”

Neno “token” hasa katika blockchain linasimama kama project yoyote ambayo inatengenezwa juu ya blockchain nyingine ,mfano LINK,COMP,DAI n.k  ni tokens kwasababu zimetengenezwa kupitia ethereum blockchain

Hivyo basi NFT ni project yoyote ambayo inakuwa katika mfumo wa picha,video au sauti(audio) ambayo haiwezi kubadilishwa na chochote kwa asilimia 100

 

NFT ni digital asset ambayo inatengenezwa kupitia blockchain ,na mtu anayeitengeneza basi ndiye anakuwa mmiliki halali pekee ,hii ikitokana na uwepo wa cryptographic codes na metadata ambazo zinatofautisha NFT moja na nyingine

 

Tofauti ya NFTs na Cryptocurrencies

Ni kweli kwamba NFT na Cryptocurrency zote zinatengenezwa katika teknolojia ya blockchain ,lakini matumizi yake ni tofauti kabisa

 

Cryptocurrency ni fungible coin/token ambazo zinaweza kuwa traded au kubadilishana ,kwa mfano una uwezo wa kumtumia mtu pesa katika dollar na aka exchgange na kupata bitcoins kadhaa

NFTs haziwezi haziwezi kuwa traded au kumpa mtu mwingi umiliki wa asilimia 100 na hivyo basi hata ukinunua NFT bado mmiliki wa kwanza atatakiwa kulipwa kama utauza NFT hiyo pia

 

NFTs zinaweza kurepresent asset Fulani ambayo inapatikana duniani na ikawa na thamani ,mfano muziki unaweza kuwa minted na kuwa NFT na kuuzwa kupitia websites ambazo kufikia mwaka 2022 zitakuwa nyingi sana na hivyo mwanamuziki kupata asilimia yake kwa kila atakayeuza muziki wake huo

 

Cryptocurrencies zinatumika kama medium of transactions na sio kama proof of ownership na hivyo hakuna mmiliki wa asilimia zote na kama utauza cryptos kadhaa hauwezi kupewa royalties

 

Royalties ni nini?

Hiki ni kiasi cha asilimia ambayo mmiliki wa NFT husika hulipwa

 

Matumizi makubwa ya NFTs

NFTs tayari zimeanza kutumika kama sehemu ya kuingiza pesa kupitia market places za NFTs nyingi tu kama Opensea na Rarible

Projects kama bored ape yatch club na cryptopunks ziliwezwa kununuliwa kwa wingi sana na kutokana na potential ya kupanda thamani watu wengi waliuza na kutengeneza faida baada ya kupanda thamani

 

NFTs pia zinaweza kutumika kuonyesha mmiliki halali wa asset Fulani kupitia minting ,mfano katika virtual worlds (metaverse) eg Decentraland tayari watu wameanza kununua viwanja na ili kiwanja kisiwe na wamiliki wawili plots za viwanja vinanunuliwa katika mfumo wa NFT ili kuwa na mmiliki mmoja

 

NFTs inaweza kutumika katika digital arts ambapo wasanii wa michoro au picha ,mziki na video wanaweza kuongeza kipato na kupunguza wizi ambao unatokana na watu kucopy kazi zao na kuuza bila wao kupata royalt yoyote

 

Vikwazo katika kununua NFTs

Kikwazo kikubwa katika NFTs ni gas fees,yaani makato hasa wakati wa ununuaji wa NFT husika katika blockchain hasa NFTs ambazo zinakuwa zimetengenezwa katika blockchain ya ethereum ,hii inafanya watu wengi kushindwa kumudu gharama zake

 

Kupitia opensea mtu yeyote anaweza jumint NFT yake bure kama atatumia polygon blockchain na lazy minting katika upande wa rarible.com

 

Ukweli ni kuwa NFTs nyingi zenye potentials kubwa bado zinatengenezwa katika ethereum blockchain

 

Wito

Kama wewe physical artist basi unaweza kuingia katika digital arts na kutengeneza pesa nzuri tu,hii inajumuisha pia wapiga picha ,wachoraji na wasanii lakini pia kampuni kubwa zenye brand ya kutosha wanaweza kuturn bidhaa zao kuwa katika NFT

 

Makampuni makubwa kama Adidas, cocacola,Nike,pepsi n.k wameshaaanza kutengeneza NFTs za bidhaa zao

 

Wasanii na watu maarufu kama Gary vee ambaye katengeneza Zaidi ya dola milioni 20, snoop dog ,Paul Regan,the weekend na wengine tayari wanatengeneza kipato kupitia NFTs

 

LENGO LA KUANDIKA MAKALA HII NI KUWAFUNGUA WATANZANIA KATIKA FURSA HIZI ZINAZOTOKANA NA BLOCKCHAIN

 

NFT marketplaces

Rarible.com   

Opensea.com

Binance NFT market place

 

Unaweza kunifatilia katika youtube na hapa pia .ili kufdahamu jinsi ya kufungua account kununua na kuuza NFT

 

WRITTEN BY : FradoFX  23/12/2021

 

 

 

 

 

Reactions

Post a Comment

1 Comments

  1. Wilkie instantly started forging ties with Xenophon as soon because it was apparent that he was elected. The territory of Puerto Rico locations significant restrictions on slot machine possession, however the regulation is widely flouted and slot machines are widespread in bars and coffeeshops. Weight count is an American term referring to the whole worth of coins 메리트카지노 or tokens removed from a slot machine's drop bucket or drop box for counting by the casino's exhausting count staff by way of the use of of} a weigh scale.

    ReplyDelete