Mambo ya msingi kabla hujaanza biashara ya forex

Mambo ya Msingi kabla hujaanza biashara ya forex 

Kama ilivyo kawaida kabla hujaanza kufanya biashara yoyote unatakiwa kuifahamu kiundani

Katika Forex pia ni hivyohivyo , ukiingia kichwa kichwa basi utakula za uso,kabla ya kuanza forex unatakiwa kufahamu mambo haya yafuatayo 

1. Forex ni biashara sio betting 
Ukishalifahamu hili tu ni hatua ya kwanza, kama unataka kufanikiwa basi unatakiwa kujua kuwa forex sio mchezo, forex ni biashara na hivyo inahitaji taalumu, inahitaji kujifunza 

Unapaswa kujisomea kama ilivyo katika profession zingine,huwezi kuendesha ndege kama hujasomea urubani au kufundishwa, huwezi kufanya biashara kama wewe mwenyewe huijui kwa ndani, hivyohivyo katika forex unatakiwa kusoma vitabu lakini pia kujifunza kupitia watu kama mimi (Mentors )

2. Forex haiwezi kukufanya tajirI haraka tu 
Kuanza kuona faida katika forex itachukua muda sio wiki sio mwezi, hili ni jambo la msingi zaidi, kupitia  makosa  unayopitia  basi unaweza kujifunza na kuendelea ku improve kila siku 

Itakuchukua muda kuyafanya yale uliyosoma kuanza kukupa faida na hivyo basi ni vyema ufahamu kuwa ni biashara ambayo inahitaji moyo sana na kama ni mtu wa kukata tamaa haraka basi utakuwa safari ngumu sana kwako 

3. Kujiunga forex
Ili kufanya forex unatakiwa kuwa na smartphone au COMPUTER na kisha downlaod trading platform kama vile meta trader 4 ,meta trader 5 n.k ,baada ya kuwa umefungua account katika website ya broker 

ILI kujiunga forex hakikisha una maarifa ya kutosha na unafahamu soko kwa undani 

KUMBUKA : Forex sio mchezo ni biashara ,Unaweza kutengeneza faida kubwa sana ukiwa na maarifa sahihi lakini pia ukapoteza pesa kama utakosa maarifa sahihi 

Unaweza kupakua kitabu changu ambacho kimeelezea kwa undani jinsi ya kutengeneza faida katika forex  ,wasiliana WhatsApp 0754958520 

TAFADHALI HAKIKISHA UMESUBSCRIBE BY EMAIL BLOG HII ILI UPATE MAFUNZO YOTE KATIKA EMAIL YAKO 

Reactions

Post a Comment

0 Comments