Kama hujawahi kufanya jambo hili katika Forex basi sio Trader

Kama jambo hili hujawahi kabisa kulifanya katika forex basi huna budi kukaa kimya 


Kabla sijakuambia jambo lenyewe kwanza unatakiwa kufahamu kuwa trader yoyote katika forex anapitia hatua mbalimbali, kwanza kabisa hatua ya kwanza ni kushindwa kufahamu ni wapi unaanzia 


Pili, kuanza kusoma na badae kujiona umeifahamu forex ndani nje, hii inakuwa kabla hata hujaweka pesa, yaaani kiufupi forex ni tamu katika kitabu kuliko katika meta trader 


Tatu, ni kuweka pesa katika real account na hapa unaanza kupata vichapo ila usikate tamaa endelea kukaza, endelea kujifunza usikate tamaa ,hapa utapata hasara na faida, utaunguza account lakini usikate tamaa 


Turudi kwenye swala la msingi, na hili swala ntalisema kwasababu kuna rafiki yangu mmoja tulijuana A level na wiki iliyopita nilipost charts na yeye chap jioni yake akanipigia simu 


Alijisifu sana kwamba yeye forex anaijua sana na kwamba alikuwa hajui kama na mimi nimeanza kufanya Namba yangu alipoteza so hakuwah kuona status kwa muda kidogo, 


Alijisifia sana kwamba amesoma vitabu karibu vyote vya forex,ANAIJUA forex ndani nje, sikuwa na maneno mengi kama kawaida, baada ya kuwa amejisifu sana nilimuuliza tu mara ya mwisho KUWITHDRAW pesa ilikuwa lini, Huyu Rafiki kumbe alikuwa hajawahi hata kudeposit pesa katika real account 


Kesho yake pia aliendelea kujisifu, ikabidi nimwambie ukweli kwamba, ukitaka kujisifu siku nyingine uwe ume withdraw hata Laki 1 then tutazungumza, Alijisifu sana na akaamua kuweka pesa 


Tangu kaweka pesa kazi yake ni kupiga simu analalamika Kwamba nimshauri afanye nini, lakin kiufupi  sikupenda tabia yake na hii ipo kwa newbies wengi sana TUNATAKA WITHDRAW na sio DEPOSIT 


Reactions

Post a Comment

0 Comments